Storm FM

Watendaji Geita walioondoka na michango ya wananchi watakiwa kuirudisha

16 November 2023, 12:56 pm

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita wakiwa katika kikao cha Baraza la madiwani. Picha na Mrisho Sadick

Baadhi ya watendaji wa vijiji katika Halmashauri ya wilaya ya Geita kuhama na michango ya wananchi kumezua maswali huku wananchi wakiomba kurudishiwa fedha zao.

Na Mrisho Sadick – Geita

Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Geita kuwarudisha vituo vyao vya kazi watendaji wote wanaodaiwa kuondoka na fedha za michango ya wananchi baada ya kuhamishiwa vituo vingine vya kazi.

Magembe ametoa maagizo hayo kwenye kikao Cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Geita baada ya kupokea malalamiko Kutoka kwa wananchi wa vijiji vya Ntono na Ikina wilayani humo kuwa watendaji wa vijiji hivyo wameondoka na michango ya wananchi baada ya kuhamishwa vituo vya kazi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Geita

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Charles Kazungu amesema anatambua uwepo wa changamoto ya watendaji hao na ameshaielekeza Halmashauri hiyo kuchukua hatua hatua ikiwemo ya kuwataka watendaji kurudisha fedha za wananchi.

Kushoto ni Mkuu wilaya ya Geita Cornel Magembe na kulia ni Charles Kazungu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita wakiwa katika kikao cha Baraza la madiwani. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo wameunga Mkono maagizo hayo huku Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita Barnabas Mapande akiwataka madiwani kushirikiana na watendaji ili kuondoa changamoto kama hizo.

Sauti ya Madiwani na Mwenyekiti wa CCM