Storm FM

UVCCM Geita yaahidi kusimamia fedha za 10%

22 April 2024, 5:58 pm

Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Geita Ndg. Manjale Magambo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Kale Chongela

Baada ya Serikali kupitia Wizara ya TAMISEMI kutangaza kurejesha mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, UVCCM mkoa wa Geita yaagiza Halmashauri za Geita kutenda haki kwenye utoaji wa mikopo hiyo.

Na Kale Chongela – Geita

Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM mkoa wa Geita Ndg. Manjale Magambo ameagiza halmashauri zote za mkoa wa Geita kusimamia vyema fedha za asilimia 10 ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan ili ziwafikie walegwa.

Amesema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM mkoa wa Geita zilizopo mtaa wa Magogo ambapo amesema baada ya kusitishwa kwa  muda hatimaye serikali imerejesha  fedha hizo na mgawanyo wake ukiwa ni asilimia 4 kwa vijana, asilimia 4 kwa wanawake na asilimia 2 kwa watu wenye ulemavu.

Sauti ya Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Geita

Aidha ameongeza kuwa ufatiliaji wa fedha hizo utaenda sambamba na ufatiliaji wa vikundi vyote vya halmashauri za mkoa wa Geita ili kuondoa changamoto ya uwepo wa vikundi hewa ambavyo vinarudisha nyuma malengo ya serikali

Sauti ya Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Geita

Kwa upande wao baaadhi ya vijana akiwemo katibu wa wamesema ili vijana waweze kujikwamu kiuchumi kuna haja ya kila kijana kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo  na kwamba ni vyema ikatumika kwa matumizi yaliyo sahihi na kwa matumizi mengine tofauti .

Sauti ya baadhi ya vijana