Storm FM
Storm FM
5 June 2026, 7:30 pm

Jumla ya wanafunzi 77 wa darasa la saba walifanya mtihani huo, ambapo wanafunzi 76 walipata wastani wa A na mwanafunzi mmoja pekee akipata wastani wa B.
Na: Ester Mabula
Shule ya Royal Family English Medium Primary School iliyopo mkoani Geita imeendelea kung’ara kitaaluma baada ya kuongoza katika matokeo ya mtihani wa Mock wa Kanda ya Ziwa, huku wanafunzi wote wa kike walioshiriki mtihani huo wakifanikiwa kupata wastani wa daraja A.
Katika matokeo hayo, shule hiyo imeibuka mshindi wa kwanza katika Manispaa ya Geita kati ya shule 91 zilizoshiriki mtihani huo.
Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Mkurugenzi wa shule hiyo Mhandisi Lazaro Philipo amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mkubwa kati ya walimu, wazazi na wanafunzi pamoja na nidhamu ya hali ya juu katika kufundisha na kujifunza.

Ameishukuru jamii kwa kuendelea kuiamini Royal Family English Medium Primary School na kuahidi kuongeza juhudi zaidi ili kuifanya shule hiyo kuwa kitovu cha elimu bora na maadili mema nchini.