Storm FM

GGML kuendeleza mapambano ya VVU kupitia Kili challenge 2026

12 July 2026, 7:08 am

Kaimu mkurugenzi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML), Duan Campbell aizungumza katika maadhimisho ya Geita Afya day. Picha na Ester Mabula

GGML Kili Challenge ilianzishwa mwaka 2001 na Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini Tanzania.

Na: Ester Mabula

Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) umeendelea kushirikiana na Serikali kuunga mkono juhudi za kupambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kupitia utoaji wa elimu, upimaji wa VVU na kuhamasisha jamii kuondokana na unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na  maambukizi ya VVU nchini.

Kupitia zoezi la GGML Kili Challenge mwaka huu 2026, jumla ya vijana 50 wakiwemo wafanyakazi wa mgodi huo watapanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuhamasisha jamii kuhusu mapambano dhidi ya VVU pamoja na kuchangisha fedha za kusaidia shughuli mbalimbali za mapambano hayo.

Katibu tawala wilaya ya Geita Bi. Lucy Beda, mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Geita akizungumza.

Akizungumza mgeni rasmi, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Geita katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Jamii Mkoa wa Geita mwaka 2026, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Lucy Beda, amesema Serikali inathamini ushirikiano wa wadau kama GGML katika kuimarisha afya ya jamii

Sauti ya mgeni rasmi Katibu tawala Bi. Lucy Beda

Kaimu mkurugenzi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML), Duan Campbell, amewashukuru wadau mbalimbali kwa kushirikiana kufanikisha Kili Challenge 2026, huku akiahidi kuwa mgodi huo utaendelea kushirikiana na jamii katika masuala ya afya na maendeleo.

Sauti ya Kaimu mkurugenzi wa GGML Duan Campbell

Mganga mkuu wa mkoa wa Geita Dkt. Omary Sukari amesema kuwa mkoa wa Geita unakadiriwa kuwa na wagonjwa wa WAVIU 95,000 huku baadhi ya washiriki wa Kili challenge wakieleza matarajio yao.

Sauti ya mganga mkuu wa mkoa wa Geita Dkt. Omary Sukari
Sauti ya washiriki wa Kili challenge 2026
Baadhi ya washiriki wa matembezi na mbio katika maadhimisho ya Geita Afya day. Picha na Ester Mabula

Maadhimisho hayo yaliambatana na matembezi ya afya, zoezi la uchangiaji damu pamoja na kuaga rasmi wawakilishi 50 kutoka Mkoa wa Geita watakaoshiriki kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia Kili Challenge kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia mapambano dhidi ya VVU ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Kuwa na mwenza mmoja, tulia”.