Storm FM
Storm FM
6 May 2026, 1:03 pm

Kila Jumatano ya kwanza ya kila mwezi (EWURA) Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini hutangaza bei mpya kikomo za mafuta zitakazotumika kwa mwezi husika.
Na: Ester Mabula
Watumiaji wa mafuta mkoani Geita wameendelea kulalamikia kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, hali inayosababisha ongezeko la gharama za maisha kwa wananchi.
Wananchi hao hususani madereva wa vyombo vya usafiri wanasema ongezeko hilo limepunguza faida na kuongeza gharama ya nauli kwa wateja kwani wamelazimika kupandisha nauli ili kuendana na hali ya soko.
Kwa mujibu wa Afisa kutoka baraza la ushauri mkoa wa Geita (EWURA CCC) Bw. Wadi Omary amesema bei za mafuta zimeongezeka katika mikoa mbalimbali nchini na si mkoa wa Geita pekee bali na hali ya kidunia.
Kwa mkoa wa Geita bei za mafuta ambazo zitatumika kwa mwezi huu wa tano ni kama ifuatavyo;
Wilaya ya Geita Petroli ni 4,315 na Dizeli ni 4,499 kwa lita moja.
Wilaya ya Bukombe Petroli ni 4,304 na Dizeli ni 4,438 kwa lita moja.
Wilaya ya Chato Petroli ni 4,336 na Dizeli ni 4,470 kwa lita moja.
Wilaya ya Mbogwe Petroli ni 4,354 na Dizeli ni 4,487 kwa lita moja.
Wilaya ya Nyang’hwale Petrol ni 4,330 na Dizeli ni 4,464 kwa lita moja.
Utofauti wa bei za mwezi huu wa tano na bei za mwezi uliopita wa Aprili ni kama ifuatavyo:
Geita Petroli ilikuwa 4,020 na Dizeli 4006 kwa lita moja.
Bukombe Petroli ilikuwa 4,009 na Dizeli 3,995 kwa lita moja.
Chato Petroli ilikuwa 4,041 na Dizeli 4,027 kwa lita moja.
Mbogwe Petroli ilikuwa 4,058 na Dizeli 4,044 kwa lita moja.
Nyang’hwale Petroli ilikuwa 4,035 na Dizeli 4,021 kwa lita moja