Storm FM

Bweni laungua moto wanafunzi watano wakimbizwa hospitali

25 October 2023, 10:29 am

Sehemu ya uharibifu wa uliyosababishwa na moto katika bweni la shule ya sekondari Queen Marry . Picha na Evance Mlyakado

Wananchi wengi hawajui namna ya kupambana na moto pindi unapozuka kwenye nyumba zao hata kama kuna vifaa vya kuzimia moto huku serikali ikishauriwa kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi.

Na Mrisho Sadick:

Bweni la wasichana shule ya sekondari Queen Marry of Peace inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Geita limeungua moto na kusababisha uharibifu wa jengo hilo, pamoja na hasara ya vifaa mbalimbali vya wanafaunzi wanaolala katika bweni hilo, ikiwemo vitanda na magodoro.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita, Shaban Dawa amesema walifanikiwa kuuzima moto huo huku wanafunzi watano wakikimbizwa hospitali kutokana na mshituko walioupta kutokana na taharuki kwa wanafunzi wa shule hiyo na kusababisha hasara ya kuteketea kwa vitanda, magororo, vifaa binafsi vya wanafunzi pamoja na uharibifu wa jengo na kwamba wanaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha moto huo.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa na vitu vilivyookolewa kwenye bweni la shule ya sekondari Queen Marry. lililoungua moto. Picha na Evance Mlyakado
Sauti ya Kamanda wa Zimamoto

Kwa upende katibu wa Askofu Jimbo la Geita Yohane Mabula licha ya kusikitishwa na ajali hiyo ya moto ambayo imesababisha hasara na taharuki kwa wanafunzi, amewataka wanafunzi hao, kuwa watulivu wakati serikali ikiendelea na taratibu nyingine, ikiwemo kuchunguza chanzo cha ajali hiyo pamoja na kukarabati jengo hilo.

Sauti ya Katibu wa Askof Jimbo la Geita