Storm FM

Migogoro ya ardhi suluhisho lake ni lipi?

6 July 2023, 8:47 am

Wakazi kata ya Nyankumbu katika mgogoro wa ardhi. Picha na Kale Chongela

Moja ya changamoto inayojitokeza mara kwa mara katika maeneo tofauti ya mkoa wa Geita ni migogoro ya ardhi, wananchi wamefunguka ili kupata ufumbuzi.

Baadhi ya wakazi wa kata ya Nyankumbu wameiomba serikali ya wilaya ya Geita kutatua Migogoro ya ardhi ambayo imetajwa kuwa changamoto kwao .

Wamesema hayo kufuatia kuwepo kwa mgogoro  wa ardhi uliotokea katika mtaa wa Uwanja baina ya watu wawili, kumiliki hati ya kiwanja katika eneo moja jambo ambalo limeibua sintofahamu.

Sauti ya Wakazi kata ya Nyankumbu wakizungumzia mgogoro wa ardhi.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Cornel Magembe akizungumza kwa njia ya simu   amekiri kupokea malalamiko hayo katika ofisi yake ambapo ametoa maagizo kwa afisa ardhi kutoka ofis ya Mkurugenzi kuhakikisha anatatua changamoto hiyo.