Storm FM

Mtoto alishwa kinyesi Ikulwa.

3 August 2021, 2:19 pm

Na Zubeda Handrish:

Mtoto wa darasa la nne ambaye ni mkazi wa kata ya Ikulwa mkoani Geita anadaiwa kulishwa kinyesi na mama yake mlezi (wa kambo) ikisemekana chanzo ni ugomvi wa wazazi.

Afisa maendeleo katika kata hiyo Bi. Tabisa James Yawanga amesikitishwa na tukio hilo, mara baada ya kuzungumza na mama huyo na kukiri kufanya kitendo hicho na kuanza kulishughulikia suala hilo kwa kumuamisha mtoto huyo kwa kushirikiana na wakazi wa eneo hilo.