Storm FM
Storm FM
14 October 2026, 12:11 pm

Muonekano wa mtaro uliochimbwa katika mtaa wa mwatulole. Picha na Kale Chongela
Na: Kale Chonbgela
Geita imeanza jitihada za kuchimba mitaro kwa lengo la kurahisisha upitishaji wa maji ya mvua na kuzuia maji hayo kutuama katika maeneo ya makazi ya wananchi.
Serikali ya Mtaa wa Mwatulole Kata ya Buhalahala Halmashauri ya manispaa ya Geita imeanza jitihada za kuchimba mitaro kwa lengo la kurahisisha upitishaji wa maji ya mvua na kuzuia maji hayo kutuama katika maeneo ya makazi ya wananchi mtaa huo.
Akizungumza na Storm Fm Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw Edward Misalaba amesema hatua hiyo inalenga kuboresha mfumo wa upitishaji wa maji katika mtaa huo ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na maji ya mvua
Sauti ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mwatulole
Aidha Wananchi wanahimizwa kuendelea kushirikiana na viongozi wa mtaa katika kuhakikisha mitaro hiyo inatunzwa na haizibwi kwa taka na inaendelea kuruhusu maji kupita kwa urahisi.
Sauti ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mwatulole

Muonekano wa mtaro uliochimbwa katika mtaa wa mwatulole. Picha na Kale Chongela
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo ametumia fursa hiyo kwa kupongeza jhatua huku wakibainisha kuwa mitari hiyo inaenda kusaidi hasa kipindi cha mvua .
Sauti ya wananchi