Storm FM

Tetemeko la ardhi lasababisha athari Manispaa ya Geita

10 November 2026, 6:16 pm

Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani. Picha na Mrisho Sadick

Tetemeko la kwanza lilikuwa na mgandamizo wa 5.1 na lapili lilikuwa na mgandamizo wa 4.6 katika kipimo cha Richter ambayo yalitokea Manispaa ya Geita

Na Mrisho Sadick

Halmashauri ya Manispaa ya Geita mkoani Geita imewataka wananchi kutoa taarifa kuhusu athari zozote zilizojitokeza katika maeneo yao kufuatia matetemeko mawili ya ardhi yaliyotokea Novemba 5 na 9 mwaka huu.

Akizungumza leo Novemba 10,2026 katika kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Geita Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Yefred Myenzi amesema matetemeko hayo yamesababisha athari kidogo katika baadhi ya miundombinu ya umma ikiwemo Shule ya Msingi Juhudi.

Myenzi amesema tetemeko la kwanza lilikuwa na mgandamizo wa 5.1 lapili lilikuwa na mgandamizo wa 4.6 katika kipimo cha Richter huku akiwataka wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika iwapo wamebaini uharibifu wowote katika makazi, majengo au miundombinu mingine ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Sauti ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita