Storm FM

Kampeni ya ongea na kamanda kuwa mwarobaini wa changamoto za bodaboda Geita

14 October 2026, 2:32 pm

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Safia Jongo. Picha na Kale Chongela

Kampeni hiyo iliyopewa jina la ONGEA NA KAMANDA yenye lengo la kuwawezesha wananchi kuwasilisha kero na changamoto zinazowakabili ili zipatiwe ufumbuzi.

Na: Kale Chongela

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Safia Jongo ameanzisha kampeni iliyopewa jina la ONGEA NA KAMANDA yenye lengo la kuwawezesha wananchi kuwasilisha kero na changamoto zinazowakabili ili zipatiwe ufumbuzi.

Kamanda Jongo akiwa katika ukumbi wa Bwalo la Polisi  manispaa ya Geita akizungumza na maafisa usafirishaji amesema kampeni hiyo inalenga kuimarisha mawasiliano mazuri kati ya Serikali na wananchi wake kwa kuwapa fursa ya kueleza changamoto zao na kupata ufumbuzi kwa wakati.

Sauti ya kamanda Safia Jongo

Kwa upande wake mwenyekiti wa Umoja wa waendesha bodaboda Mkoa wa Geita Fred Fidel amesema  kampeni hiyo imewapa fursa ya kila bodaboda kuwasilisha kero yake na iweze kupatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Sauti ya mwenyekiti wa umoja wa waendesha bodaboda Geita

Picha ya maafisa usafirishaji Halmashauri ya manispaa ya Geita. Picha na Kale Chongela

Kwa upande wake Bw, Hanschadius Valentine kwa niaba ya Maafisa usafirishaji Halmashauri ya manispaa ya Geita amepongeza kampeni hiyo kwani ni mwarobaini wa changamoto zinazowakabili.

Sauti ya mmoja wa maafisa usafirishaji