Storm FM

TANROADS Geita yaimarisha miundombinu kukabiliana na mvua za El Nino

8 October 2026, 1:50 pm

Picha baadhi ya wafanyakazi wa TANROADS wakifungua midomo ya Daraja kwaajili ya kupitisha maji. Picha na Ashura Ramadhani

Na: Ashura Ramadhani

Mitaro imechimbwa ili kuelekeza maji katika maeneo salama, huku Barabara ya Mtakuja–Bukoli, eneo la Nyarugusu, ikiendelea kufanyiwa kazi kwa kujenga kuta na mitaro ya kuzuia maji kuvuka barabara.

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Geita imechukua hatua za kuimarisha miundombinu ya barabara katika maeneo hatarishi kwa mvua, ikiwemo kufungua midomo ya Daraja la Nyikonga, kusafisha njia ya mto na kuelekeza mkondo wa maji katika Barabara ya Katoro–Ushirombo.

Akizungumza Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita, Mhandisi Hosea Machaka, amesema katika eneo la Katoro mitaro imechimbwa ili kuelekeza maji katika maeneo salama, huku Barabara ya Mtakuja–Bukoli, eneo la Nyarugusu, ikiendelea kufanyiwa kazi kwa kujenga kuta na mitaro ya kuzuia maji kuvuka barabara.

Sauti ya kaimu meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita

Picha ya kaimu meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita. Picha na Ashura Ramadhani

Msimamizi wa Kitengo cha Mipango TANROADS Geita, Mhandisi Sabato Manyinyi, amesema ongezeko la shughuli za kilimo na makazi limeongeza mtiririko wa maji kuelekea barabarani, hali inayoweza kuhatarisha miundombinu na usafiri.

Amesema TANROADS inaendelea kutumia makalavati ya dharura aina ya CMP, kusafisha na kuelekeza njia za mito, pamoja na kuongeza njia za maji katika maeneo hatarishi.

Sauti ya msimamizi kitengo cha mipango TANROADS Geita

Picha ikionyesha miongoni mwa daraja lililofanyiwa ukarabati kwaajili ya kupitisha maji. Picha na Ashura Ramadhani