Storm FM

Maandalizi tamasha la utamaduni na nyama choma yafikia 95%

21 May 2026, 2:03 pm

Ngoma ya asili ya kabila la walongo ambao ndiyo wazawa wa mkoa wa Geita. Picha na Ester Mabula

“Tamasha hili sio tu litawakutanisha watu pamoja bali pia litaenzi mila na desturi zetu sambamba na kuongeza uchumi wa wananchi wa Geita” – Mkurugenzi Yefred Myenzi

Na: Ester Mabula

Kuelekea tamasha la Utamaduni na Nyamachoma litakalofanyika kwa muda wa siku mbili Mei 22-23, 2026 katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu zamani EPZA manispaa ya Geita, Mkurugenzi wa manispaa ya Geita Yefred Myenzi amesema lengo kuu la Tamasha hilo ni kuwakutanisha watu pamoja baada ya kazi ili kuendelea kuenzi utamaduni wa asili pamoja na kujifunza mambo mbalimbali.

Sauti ya mkurugenzi manispaa ya Geita Yefred Myenzi
Mkurugenzi wa manispaa ya Geita Yefred Myenzi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

Akizungumza Afisa Utamaduni manispaa ya Geita Bi.  Sia Kisamo amesema tamasha hilo ni mahsusi kwaajili ya kuwarudisha watu katika asili pamoja na kuwakumbusha tamaduni nzuri ambapo pia kutakuwa na kitabu cha asili ya kabila la walongo na mkoa wa Geita kwa ujumla ambacho kitatolewa bure ili kujifunza zaidi historia.

Sauti ya Afisa utamaduni Bi. Sia Kisamo
Afisa utamaduni manispaa ya Geita Bi. Sia Kisamo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Bw. Sostenes Mbwilo amesema maandalizi yamefikia asilimia 95 na kuwaomba wajasiriamali pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi kwani kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa asili pamoja na kizazi kipya.

Sauti ya mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Sostenes Mbwilo

Tamasha hilo la utamaduni kwa mwaka huu 2026 limepewa kauli mbiu isemayo “Onja Utamaduni, Ishi katika Mdundo wake”.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Sostenes Mbwilo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula