Storm FM

Polisi: Hakuna malipo kupata dhamana

30 January 2024, 12:46 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo akiwa kwenye Kipindi cha Storm Asubuhi cha Storm FM. Picha na Kale Chongela

Kutokana na uwepo wa malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa huwezi kupata mdhamana kutoka polisi bila kutoa rushwa jeshi la polisi limekanusha taarifa hizo.

Na Mrisho Shabani:

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita kamishna msaidizi wa polisi ACP Safia Jongo amewataka wananchi kuacha tabia ya kutoa rushwa kwenye vituo vya polisi ili wapate dhamana kwakuwa dhamana ni bure.

Kamanda Jongo ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano maalumu ya kipindi cha Storm Asubuhi cha Storm FM ambapo amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inaongozwa kwa misingi ya utawala bora

Amesema Jeshi hilo limeendelea kuwachukulia hatua baadhi ya askari wanaofanya kazi kinyume cha sheria huku akiwataka wananchi kutoa taarifa kwake pindi wanapokutana na changamoto ya kuombwa rushwa ili wapate huduma za kipolisi kama dhamana.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Geita

Sanjari na hayo ametumia fursa hiyo kwa kuwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiana kwa jeshi la Polisi katika kufichua baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili sambamba na wanaofanya vitendo vya uharifu.