Storm FM

Ngo’mbe wawili wamekufa baada ya kunywa maji yenye sumu Geita

23 April 2021, 6:07 pm

Na Kale Chongela:

Ng’ombe wawili wamekufa baada ya kunywa maji yenye sumu kutokana na kutapakaa kwa maji yenye sumu yanayo toka katika eneo la uchenjuaji wa madini ya dhahabu    katika mtaa wa Samina Kata ya Mtakuja Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita.

Akizungumza na Storm Fm kwa njia ya simu  Daktari wa mifugo wa Halmashauri ya mji wa Geita  Jasson Mutayabarwa  amethibitisha kutokea kwa   tukio hilo baada ya uchunguzi wa sampuli ya maji hayo ambapo amebaini  sumu kuathiri baadhi ya viungo vya ng’ombe hao nakuwasababishia kifo.

Daktari wa Mifugo Geita

Mmiliki wa ng’ombe waliokufa Bw Godson Luvugo   ambaye ni mkazi wa eneo la Samina ameuomba uongozi wa ofisi ya madini na kata ya Mtakuja kutafta namna ya  kutatua changamoto kwani sio mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea kwenye kata hiyo.

Nae Afisa madini Mkoa wa Geita Bw Daniely Mapunda amesema atahakikisha  anasimamia sheria  kwa mujibu wa taratibu na kanuni ambazo  zinatakiwa kufuatwa na wawekezaji eneo la makazi ya watu ili kuepukana na migogoro isio kuwa ya lazima.