Storm FM

Wanawake kujifungulia barabarani ndio basi tena Mbogwe

5 August 2023, 7:54 pm

Jengo la wodi ya wazazi katika Kata ya Ilolangulu wilayani Mbogwe. Picha na Mrisho Sadick

Changamoto ya wanawake kujifungulia majumbani na barabarani huenda ikamalizika katika kata ya Ilolangulu wilayani Mbogwe baada ya serikali kujenga wodi.

Na Mrisho Sadick:

Wanawake wa kata za Ilolangulu , Isebya na Ikobe wilayani Mbogwe mkoani Geita wameondokana na adha ya kujifungulia njiani na majumbani baada ya serikali kuwajengea wodi ya wazazi ili kuokoa vifo vya kina mama wajawazito na watoto.

Mbio za mwenge wa Uhuru zimeendelea kukimbizwa Mkoani Geita na zimefika katika mradi wa Jengo la wodi ya Wazazi katika Kata ya Ilolangulu wilayani Mbogwe huku wakazi wa maeneo hayo Ester Robert na Shukuru Petro wakisema hatua hiyo itasaidia kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto.

Sauti ya wananchi wa Kata ya Ilolangulu

Awali akitoa taarifa ya mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ilolangulu Sospeter Manjala amesema zahati hiyo inahudumia watu zaidi ya elfu 40 kutoka Kata tatu nakwamba Jengo hilo liko sambamba na ujenzi wa Ofisi ya wauguzi,vyoo vitatu, bafu tatu na limejengwa kwa thamani  ya zaidi ya Shilingi milioni 57 huku akitaja wastani wa idadi ya wanawake wanao jifungua kwa siku nikuanzia wawili hadi wanne.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib aliye katikati akizungumza na wananchi wa Ilolangulu Mbogwe. Picha na Mrisho Sadick

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib ameridhishwa na Utekelezaji wa mradi huo nakutoa siku nne za kufanyika marekebisho katika dosari zilizobainika.

Sauti Abdalla Shaib Kaim