Storm FM

Vibaka wabomoa ghala la chakula Mbogwe

10 July 2023, 7:20 pm

Ghala la mahindi na mpunga ambalo wezi wamebomoa na kuiba. Picha na Nicolaus Lyankando

Wezi katika maeneo mbalimbali mkoani Geita bado ni changamoto huku uongozi katika ngazi mbalimbali ukiendelea kushirikiana na wananchi kwa ukaribu ili kutokomeza vitendo hivyo.

Nicolaus Lyankando- Geita

Kundi la watu ambao hawakufahamika wamebomoa ghala la chakula na kuiba magunia ya mpunga na mahindi katika kijiji cha Mwingilo wilayani Mbogwe mkoani Geita. Akizungumzia tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia jana Julai 9, 2023 huku mmiliki wa mali iliyoibwa Paulo Maliatabu amesema tukio hilo kwake limeacha jeraha kubwa katika biashara yake na kuiomba serikali ya kijiji kuangalia namna ya kuweka ulinzi ili kukomesha matukio hayo.

Sauti ya mhanga wa tukio la wizi wa mahindi na mpunga Paulo Maliatabu

Nao baadhi ya wananchi wamelaani kitendo hicho huku wakisema watu wakikamatwa wachukuliwe hatua kali za kisheria ili liwe funzo kwa wanaofanya vitendo hivyo.

Sauti ya wananchi waliozungumza katika tukio la wizi wa mahindi na mpunga

Baada ya kuutafuta uongozi wa serikali ya kijiji hicho kupitia Mwenyekiti wa kijiji umedai wao bado hawajafikishiwa taarifa za tukio hilo hivyo wakaahidi kulifuatilia na akaelezea mikakati waliyonayo katika kukomesha vitendo hivyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Mwingilo Zakaria Magigima akizungumza kwa njia ya simu