Storm FM

Maji ya chumvi ni kero, mkuu wa wilaya atolea ufafanuzi

23 August 2023, 11:55 am

Mkuu wa wilaya Geita akizungumza na wajumbe wa kamati ya Siasa.

Changamoto ya maji safi na salama bado ni changamoto katika baadhi ya wilaya mkoani Geita, Licha ya ukosefu wa maji akini pia chumvi ipo.

Na Kale Chongela- Geita

Wananchi wa Kijiji na Kata ya Bumwang’oko  Halmashauri ya mji wa Geita, wameiomba kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Geita kuwasaidia kutatua changamoto  ya uhaba wa maji  pamoja na maji hayo kuwa na chumvi suala ambalo linapelekea wananchi kupata shida ya maji pamoja na kuwepo kwa kisima kijijini hapo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Mjumbe Kamati ya siasa ya CCM kwenye Kata hiyo Morison Gunje, amesema pamoja na kuwekewa mradi huo wa maji kijiji hapo bado unachangamoto nyingi ikiwemo suala la chumvi na kutokutoa maji ya kutosha.

Sauti ya Mjumbe Kamati ya siasa ya CCM

Hata hivyo hoja ya maji kuwa na Chumvi imeonekana  kupamba moto…

Mhandisi Isaack  Mgeni  kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira metoa ufafanuzi juu ya madai hayo.Huku Mwenyekiti wa CCM Wilayani Geita Barnabas Mapande akifafanua juu ya suala la wingi wa maji.

Sauti ya Muhandisi wa GEUWASA

Tukamilishe na kile alichozungumza mkuu wa wilaya ya Gita Cornel Magembe kulingana na kero hiyo ya maji chumvi.

Sautu ya mkuu wa wilaya ya Geita