Storm FM

Uwekezaji wa Bandari ni salama

15 July 2023, 4:43 pm

Mbunge Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi Geita. Picha na Mrisho Sadick

Mjadala wa Serikali ya Tanzania kutaka kuingia makubaliano na serikali ya dubai kupitia Kampuni ya DP World ya uboreshaji na uendelezaji wa Bandari bado unaendelea huku wabunge wakiendelea kuwatoa hofu wananchi.

Na Mrisho Sadick:

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu amewaondoa wasi wasi wananchi wa Jimbo lake juu ya  uwekezaji wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World kwani wao kama wabunge wamezingatia kwa umakini mkataba huo.

Mbunge Kanyasu ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi kwenye kijiwe cha kahawa cha Mrumba Mjini Geita kutokana na uwepo wa mijadala mingi hususani kwenye mitandao ya kijamii juu ya uwekezaji huo.

Sauti ya Mbunge Kanyasu
Baadhi ya wakazi wa Geita mjini katika mazungumzo wa Mbunge Kanyasu . Picha na Mrisho Sadick

Amesema wao kama wabunge hawawezi kupitisha mikataba ambayo itaiweka nchi matatani nakwamba ni vyema watanzania wakatambua kuwa mkataba huo  ni njia moja wapo ya kukuza uchumi wa nchi.

Nao baadhi ya wananchi akiwemo Seleman Nkwande,  Leornad Kassim na Seleman John  wakatoa maoni yao na mtazamo juu ya Mkataba wa Bandari.

Sauti ya wananchi Geita mjini