Storm FM

Wahanga wa shambulio la paka wa ajabu wapata ahueni.

6 January 2023, 9:11 am

Na Nicolaus Lyankando:

Wananchi walioshambuliwa na Paka wa ajabu akiwemo Mtoto mwenye umri wa miaka (5) katika kitongoji cha Kilimahewa Kata ya Lulembela wilayani Mbogwe Mkoani Geita wanaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni katika Kitongoji cha Kilimahewa Kata ya Lulembela, nakuzua taharuki kwa wakazi wa eneo hilo kwakuwa paka huyo hakujulikana ametoka wapi.

Baadhi ya wahanga wa tukio hilo akiwemo mama wa Mtoto huyo wamesema baada ya mtoto wake kujeruhiwa vibaya sehemu za uso alikimbizwa katika Hosptali ya wilaya ya Bukombe kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kwasasa anaendela vizuri.

Kwa upande wake Marco Jopola ni miongoni mwa watu waliopambana na paka huyo hadi kumuua wakati akimshambulia mtoto.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kilimahewa katendele Busumabu amesema majeruhi wote wanaendelea vizuri kwasasa nakuwataka wazazi na walezi kuwa walinzi wa familia zao nasiyo kuwaacha watoto peke yao majumbani pindi wanapokwenda katika shughuli za utafutaji ikiwemo shamba.