Storm FM
Storm FM
8 August 2024, 13:36

Wakazi wa kata ya Nyarugusu halmashauri ya wilaya ya Geita wameiomba serikali kutatua changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa maji safi na salama katika kijiji hicho kwani maji wanayotumia kwa sasa yanahatarisha afya zao.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Kwa nyakati tofauti tofauti, wananchi wa kijiji cha Nyarugusu wamezungumza na Storm FM na kueleza kuwa wengi wao wanatumia maji ya visima ambayo sio salama kwani mvua ikinyesha yanachanganyikana na kemikali zinazotumika kwenye uchimbaji wa madini.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Nyarugusu Oscar Ndalawa na Charles Peter Kaimu afisa mtendaji wa kijiji cha Nyarugusu wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza mipango ya utatuzi iliyopo.

Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA wilaya ya Geita Sande Batakanwa amesema tayari serikali imeleta fedha zaidi ya milioni 720 kwaajili ya ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita 225,000.