Storm FM

Aliyejiunganishia umeme kinyemela Nkome adakwa

8 August 2025, 10:35

Mtaalamu wa umeme kutoka TANESCO akikata umeme uliounganishwa kinyemela Nkome. Picha na Edga Rwenduru

Mteja kachepusha umeme kwenye njia namba moja na njia namba tatu kwa kuunga waya moja kwa moja kwenye suplaya ya TANESCO Mpaka kwenye kiwanda.

Na Edga Rwenduru:

Shirika la umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Geita limemkamata Joseph Bhukelebe mkazi wa kijiji cha Nkome wilayani Geita kwa Tuhuma za kuiba umeme kwenye nguzo kubwa na kujiunganishia kwenye kiwanda chake cha kutengeneza Barafu.

Maafisa wa TANESCO pamoja na viongozi wa serikali ya kijiji cha Nkome wamefika katika kiwanda chake cha kutengeneza barafu na kukuta mtuhumiwa huyo akitumia umeme kinyume na utaratibu hali ambayo imesababisha uharibifu wa miundombinu na kuhujumu mapato ya Shirika hilo.

“Leo tupo hapa Nkome kiufupi kuna mteja wetu anaitwa bwana joseph tumekuta amekiuka mashariti ya TANESCO kwa kutumia umeme nje ya utaratibu amechepusha matumizi ya umeme kupitia nje ya mita na kuweka kwenye matumizi na kitendo hicho ni kinyume na utaratibu na sheria zetu kama shirika la umeme” Amesema Eleuterias Katemana afisa usalama wa TANESCO Mkoa wa Geita

Sauti ya afisa usalama wa TANESCO Geita
Maafisa wa TANESCO pamoja na viongozi wa serikali ya kijiji cha Nkome wakiwa eneo la tukio. Picha na Edga Rwenduru

Juma Mputo Charles ni Mtaalamu wa umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Geita amesema jinsi nyaya za umeme zilivyokuwa zimeungwa katika kiwanda hicho ilikuwa haioneshi kiwango halisi cha umeme unaotumika.

Sauti ya mtaalamu wa umeme TANESCO

Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Nkome Sylivester Machela amewasihi wananchi kuacha tabia ya kuchezea miundombinu ya umeme kwani ni hatari kwa maisha yao badala yake wanapoona itirafu watoe taarifa kwa wahusika

Sauti ya Mtendaji wa Kijiji cha Nkome