Storm FM

Geita Gold Queens yakwama, wadau waombwa msaada

24 August 2023, 8:30 pm

Wachezaji wa Geita Gold Queens walioipandisha timu hiyo ligi kuu wakiwa mazoezini msimu wa 2022/23. Picha na Zubeda Handrish

Ukata wa kifedha umekuwa changamoto kubwa kwa klabu mpya ya ligi kuu ya wanawake ya Geita Gold Queens ya hapa mkoani Geita, na kumuinua Mwenyekiti wa Chama cha Soka Geita kuwaomba wadau msaada.

Na Zubeda Handrish- Geita

Klabu ya wanawake ya hapa mkoani Geita iliyofanikiwa kupanda Ligi kuu kutokea Championship msimu ulioisha wa 2022/23 ya Geita Gold Qeens, hali imekuwa tofauti baada ya timu hiyo kushindwa kusajili hata mchezaji mmoja hadi sasa kwaajili ya msimu mpya.

Wachezaji wa Geita Gold Queens walioipandisha timu hiyo ligi kuu wakiwa mazoezini msimu wa 2022/23. Picha na Zubeda Handrish

Ikumbukwe Shirikisho la soka Tanzania TFF na Bodi ya Ligi Kuu TPLB siku chache zilizopita ilitoa orodha ya vilabu ambavyo havijasajili hata mchezaji mmoja hadi sasa huku Geita Gold Queens ikiwa miongoni mwao.

Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Geita GEREFA, Salumu Kulunge ametolea ufafanuzi juu ya changamoto inayoikumba klabu hiyo ya soka ya wanawake ya mkoani hapa huku akiomba wadau kujitokeza kuisaidia.

Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Geita GEREFA, Salumu Kulunge akizungumza baada ya klabu ya Geita Gold Queens kukwama kusajili wachezaji

Tukiwa tunajikumbusha katika shamra shamra za kuwapokea wana Geita Gold Queens baada ya kufanikiwa kupanda Ligi kuu, ambao huu msimu wa 23/24 ungekuwa msimu wao wa kwanza, alizungumza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Bi. Zahara Michuzi kuhusiana na hatma ya klabu hiyo ya soka ya wanawake mkoani hapa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Bi. Zahara Michuzi, akizungumza baada ya Geita Gold Queens kufuzu ligi kuu.