Storm FM

Wakazi mtaa wa Uwanja waomba shule ya upili (sekondari)

2 May 2024, 4:13 pm

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Uwanja wakiwa katika mkutano. Picha na Edga Rwenduru

Licha ya jitihada za serikali kuwekeza katika elimu kwa kujenga shule mpya na za kisasa kwa baadhi ya maeneo nchini, bado ni kitendawili kwa wakazi wa mtaa wa Uwanja kutokana na kukosa shule ya upili (sekondari).

Na: Edga Rwenduru – Geita

Wakazi wa mtaa wa Uwanja kata ya Nyankumbu halmashauri ya mji wa Geita wameiomba serikali kuwajengea shule ya sekondari katika mtaa huo kwani watoto wao wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda shule ya sekondari Rukaranga.

Wamebainisha hayo katika mkutano wa kuhitimisha ziara ya katibu mwenezi na mafunzo wa tawi hilo Sebastian Kanga wakieleza kuwa wanalazimika kuingia gharama za kuwalipianauli ya daladala kwenda na kurudi.

Sauti za wananchi wa Uwanja
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano. Picha na Edga Rwenduru

Aidha katika hatua nyingine wananchi hao wameiomba serikali kuwatengenezea barabara za mitaa ambazo zimeharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha.

Sauti za wananchi wa Uwanja
Mwenyekiti wa mtaa wa Uwanja Enos Chelehani akizungumza na wananchi kwenye mkutano. Picha na Edga Rwenduru

Mwenyekiti wa mtaa huo Enos Chelehani pamoja na Katibu mwenezi CCM tawi la uwanja Sebastiani Kanga wamesema tayari mtaa umeanza kuchukua hatua za kufanyia kazi changamoto hizo.

Sauti ya Mwenyekiti na Katibu mwenezi