Storm FM

Wananchi wahofia usalama baada ya mbwa wa ulinzi kuuliwa Msufini

15 May 2024, 11:25 am

Shughuli mbalimbali zikiendelea katika soko la Msufini mjini Geita. Picha na Storm FM

Imezoeleka kuwa mnyamba aina ya Mbwa hutumika kwa shughuli za ulinzi wa mali na binadamu hasa nyakati za usiku pindi walalapo, hali imekuwa tofauti kwa wakazi wa Msufini kata ya Kalangalala katika halmashauri ya mji wa Geita.

Na: Amon Mwakarobo – Geita

Baada ya kituo cha redio Storm FM kutoa taarifa ya malalamiko ya baadhi ya wananchi wa mtaa wa Msufini kulalamikia suala la mbwa kuzagaa maeneo ya soko la Msufini na wafanya biashara wa soko hilo kupinga malalamiko hayo wakisema mbwa hao ni walinzi wa soko.

Taarifa ya awali ya malalamiko ya wananchi ilitolewa na Storm FM Mei 10, 2024 na usiku wa kuamkia Mei 11, 2024 mbwa hao wakafa kutokana na ikile kinachoelezwa ni mnyama wa ajabu kuwashambulia.

Storm fm imezungumza na wajasiriamali na wafanya biashara sokoni hapo ambao wameeleza kusikitishwa na kitendo hicho na kuhofia maisha yao kwani wanahofu mnyama huyo anaweza kuwashambulia hata binadamu

Sauti ya wafanya biashara

Katibu wa soko hilo anayejulikana kwa jina maarufu la mama Kili amesema iwapo kuna mtu anaye ua mbwa hao aache mara moja kwani mbwa hao ni walinzi wa soko hilon na si vinginevyo.

Sauti ya katibu wa soko