

8 August 2024, 12:24 pm
Zoezi la kujiandikisha na kuboresha taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura linaendelea katika mkoa wa Geita tangu kuanza Agosti 05, 2024
Ikiwa leo ni siku ya tatu ya tangu kuanza kwa zoezi la kujiandikisha na kuboresha taarifa za wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu mwakani, halmashauri ya mji wa Geita imeandikisha zaidi ya wananchi elfu 24.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita Yefred Myenzi alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Storm asubuhi kupitia redio Storm FM ambapo amebainisha katika halmashauri ya mji wa Geita kuna jumla ya vituo 130 vya kujiandikisha.
Aidha ameeleza makundi mbalimbali ambayo yanatakiwa kujiandikisha na kubainisha pia wapo watu ambao wamepoteza sifa za kuendelea kuwepo katika daftari hilo huku akiwasihi wananchi kujitokeza katika zoezi hilo.