Storm FM

Watu 25 wakamatwa kwa tuhuma za ujangili Geita

9 November 2023, 3:34 pm

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kamishna msaidizi wa polisi ACP Safia Jongo. Picha na Kale Chongela

Matukio ya ujangili yamekithiri kiasi cha Jeshi la Polisi mkoa wa Geita kuamua kuchukua hatua za makusudi kukabiliana na hilo.

Na Kale Chongela- Geita

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limewakamata watu 25 kwa tuhuma za ujangili wa misitu ikiwemo uchomaji mkaa, uchanaji wa mbao na ulinaji asali usiyofuata utaratibu.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kamishna msaidizi wa polisi ACP Safia Jongo amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao kufuatia oparesheni maalumu ya kuelekea mwisho wa mwaka ya kupambana na vitendo vya uhalifu na ukataili wa kijinsia katika jamii.

Sauti ya Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kamishna msaidizi wa polisi ACP Safia Jongo

Kamanda Jongo amesema katika oparesheni hiyo wamefanikiwa kukamata magunia ya mkaa 410, vipande vya mbao vilivyovunwa kinyemela 1965, ngo’mbe 406, pikipiki 8, baiskeli 23 na Gari moja aina ya fuso lenye namba za usajili T-339 DZQ.