Wajasiriamali 300 wapatiwa mafunzo Geita
26 April 2021, 1:53 pm
Na Joel Maduka:
Wajasiriamali zaidi ya mia tatu waliopatiwa mafunzo na baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi, wametakiwa kutumia ujuzi ambao wamepatiwa kutazama fursa kwenye makapuni mbali mbali na kuachana dhana ya kusubili tenda katika mgodi wa dhahabu wa Geita GGML.
Wito huo umetolewa na katibu tawala wa Mkoa wa Geita Bw Denis Bandisa wakati akifungua mafunzo kwa wajasiriamali hao ambayo yamefadhiliwa na mgodi wa GGML.
Kwa upande wake Katibu mkuu mtendaji wa baraza hilo Bi Beng’i Issa amewataka wajasiriamali waliopata mafunzo hayo kwenda kujiajiri pamoja nakuanzisha viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao.
Baadhi ya wajasiriamali ambao wamepatiwa mafunzo hayo wameishukuru serikali kwa kushirikiana na Mgodi wa dhahabu wa Geita GGML kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa wakazi wa mkoa wa Geita.