Storm FM

Kata yenye wakazi zaidi ya elfu 60 haina kituo cha afya

6 July 2023, 11:42 am

Wakazi Kata ya Nyakafuru wakiwa katika mkutano wa Mbunge. Picha na Mrisho Sadick

Ukosefu wa huduma za afya za uhakika umewasukuma wananchi kuchangishana na kununua kiwanja chenye ukubwa wa zaidi ya hekari 10 nakuishinikiza serikali kuwajengea kituo cha afya.

Na Mrisho Sadick:

Zaidi ya wakazi elfu 60 wa kata ya Nyakafuru wilayani Mbogwe Mkoani Geita wanakabiliwa na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya kutokana na kata hiyo kukosa kituo cha afya.

Kilio hicho kimetolewa na Diwani wa kata hiyo Paul Edward kwaniaba ya wananchi  wake kwenye mkutano wa hadhara uliyoandaliwa na Mbunge wa viti maalumu  wa Mkoa wa Geita Mhe Rose Busiga wa kusikiliza kero mbalimba zinazowakabili wananchi.

Diwani Kata ya Nyakafuru akiwasilisha kero za wananchi wake. Picha na Mrisho Sadick

Sauti ya Diwani Kata ya Nyakafuru Paul Edward

Akijibu kuhusu changamoto hiyo Mbunge wa Viti maalumu Mhe Rose Busiga amesema kupitia bajeti kuu ya serikali iliyopitishwa hivi karibuni Bungeni itakwenda kumaliza changamoto za huduma ya afya katika eneo hilo ikiwemo kujenga kituo cha afya.

Mbunge Viti Maalumu Geita Mhe Rose Busiga. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Mbunge Viti Maalumu Geita