Storm FM

Mwandishi wa Storm FM ashinda tuzo EJAT

24 July 2023, 9:12 am

Washindi wa tuzo za EJAT. Picha na Amon Bebe

Tuzo za EJAT hutolewa kila mwaka, huku mwaka 2022 matukio ya mauaji ya walinzi mkoani Geita, yalimuinua Said Sindo kuandaa kipindi na kushindania tuzo hiyo.

Na Zubeda Handris- Geita

Mwandishi wa habari na mtangazaji wa kipindi cha Storm Asubuhi, Said Ally Sindo usiku wa Julai 22, 2023 ameshinda tuzo ya EJAT 2022/23 katika kipengele cha Haki za Binadamu upande wa Redio.

Pichani akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Dkt. Anna Henga. Picha na Amon Bebe

Saidi Sindo aliandaa kipindi cha dakika 15 kinachoangazia kwa kina mauaji ya walinzi katika vijiji na maeneo mbambali ya mitaa mjini Geita.

Sauti ya Baby Kabaya akitangaza washindi wa tuzo za EJAT
Picha na Amon Bebe

Tuzo  za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2022 zimezinduliwa mjini Bukoba  Novemba 8, 2022.

Hii ni mara ya pili kwa Tuzo hizo za kuwatambua wanahabari kwa kazi nzuri kuzinduliwa nje ya  Dar es Salaam huku Mara kwanza zilizinduliwa Tanga Septemba 28, 2019 kwa EJAT 2020.