Storm FM

Wazee waomba ushiriki kwenye vyombo vya kutoa maamuzi

7 October 2023, 5:57 pm

Wazee kutoka mikoa ya Tanzania bara wakishiriki maadhimisho ya siku ya wazee Mkoani Geita. Mrisho Sadick

Wazee nchini bado wanakabiliwa na changamoto nyingi huku suluhu ya changamoto hizo ni wazee hao kushirikishwa kikamilifu na serikali katika mambo ambayo yanawahusu.

Na Mrisho Sadick:

katikaBaraza la Wazee Nchini limeiomba serikali kuwashirikisha Wazee kwenye vyombo vya kutoa maamuzi ikiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakwenye vikao vya mabaraza ya madiwani Ili kuongeza ufanisi wa kushughulikia changamoto zao.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Taifa Lameck Sendo kwa niaba ya wazee wote nchini katika maadhimisho ya siku ya Wazee Dunia ambayo yamefanyika Kitaifa katika viwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita huku wazee hao wakiikumbusha serikali kuharakisha mchakato wa sera na sheria ya Wazee.

Sauti ya Mwenyekiti Baraza la Wazee Taifa
Waziri Dkt Doroth Gwajima akiongoza maadhimisho ya siku ya wazee duniani Mkoani Geita . Picha na Mrisho Sadick.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita Cornel Magembe amesema Mkoa wa Geita utaendelea kuwalinda nakuwathamini Wazee kwa kutatua changamoto zao.

Changamoto zingine zilizowasilishwa katika maadhimisho hayo nipamoja huduma duni za afya, baadhi ya Wazee wastafu kukosa pensheni zao, huku Waziri wa maendeleo ya Jamii jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dkt Doroth Gwajima amesema serikali iko kazini kuhakikisha inatatua changamoto zote za Wazee.

Sauti ya Waziri Dkt Gwajima

Maadhimisho hayo yamebebwa kaulimbiu isemayo ‘Uthabiti wa Wazee kwenye Dunia yenye mabadiliko’.