Storm FM

Watu watatu wafariki kwa ajali Geita, wawili watumishi wa serikali

9 October 2023, 6:03 pm

Miili miwili ya Upendo Danda na Yusuph Yohanes ikiagwa Nyumbani katika Mtaa wa Magogo. Picha na Mrisho Sadick

Ajali za barabara zimeendelea kukatisha uhai wa watu wengi , jitihada za makusudi zinahitajika ikiwemo elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto ili kupunguza matukio hayo hususani kwa waendesha pikipiki.

Na Mrisho Sadick – Geita

Watu watatu wakiwemo watumishi wawili wa serikali wamefariki Dunia baada ya kugongwa na Gari aina ya fuso lenye namba za usajili T402 AUB katika Mtaa wa Magogo Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita.

Tukio hilo limetomea usiku wa kuamkia Oktoba 08,2023 wakati watu hao walipokuwa wamebebana kwenye usafiri wa Pikipiki yenye namba za usajili MC 576 BBK ndipo wakagongwa na Gari hilo walipokuwa wakijaribu kukata kona ya Kuelekea majumbani kwao nakufariki papo hapo.

Waombolezaji wakiwa katika shughuli ya kuaga miili ya watu wawili Danda na Johanes. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Ndugu na Jirani

Waliofariki katika ajali hiyo ni Upendo Danda Afisa serikali za mitaa mwandamizi Idara ya usimamizi,  ufuatiliaji na ukaguzi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita , Emmanuel Mao Mtumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria hapo awali alikuwa Mtumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na Yusuph Yohanes ndugu wa marehemu wa Danda.

Sauti ya Wafanyakazi wenzake

Katibu tawala wa Mkoa wa Geita Mohamed Gombati amewaongoza waombolezaji katika shughuli ya kuiaga miili miwili Nyumbani kwa marehemu Danda huku Askof wa manisa ya TAG Saimon Masunga akiwataka waumini wa kanisa hilo na madhehebu mengine kujiandaa.

Sauti ya Katibu tawala Mkoa wa Geita