Storm FM

Viongozi, wananchi kijiji cha Ikunguigazi wajivunia mafanikio

21 June 2024, 10:51 am

Mwenyekiti wa kijiji cha Ikunguigazi ameandaa hafla fupi ya kujipongeza pamoja na wananchi wake kufuatia mafanikio ya kijiji yaliyopatikana kwa muda wa miaka mitano iliyopita.

Na: Nicolaus Lyankando – Geita

Mwenyekiti wa kijiji cha Ikunguigazi ameandaa hafla fupi ya kujipongeza pamoja na wananchi wake kufuatia mafanikio ya kijiji yaliyopatikana kwa muda wa miaka mitano iliyopita

Wananchi katika kijiji cha Ikunguigazi kwa kushirikiana na serikali wamefanikiwa kujenga Matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Ikunguigazi pamoja na kununua eneo kwajili ya kujenga shule mpya ya sekondari.

Hayo yamebainishwa Katika hafla fupi ya kujipongeza iliyoandaliwa na mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Jumanne Richard Manyasa June 18, 2024 na kupitia risala iliyosomwa mbele na  Afisa mtendaji wa kijiji Joshua William Kimaro ilibainisha mafanikio kadhaa ikiwemo ujenzi wa matundu 12 ya vyoo.

Sauti ya afisa mtendaji

Lakini mbali na mafanikio hayo kijiji hicho kimegubikwa na changamoto lukuki ikiwemo barabara inayounganisha mawasiliano ya kijiji hicho na kijiji cha Nyikonga kukatika hivyo wananchi wameomba kutatuliwa kero hiyo

Sauti ya wananchi
Viongozi wakijiji wakipita katika barabara iliyochimbwa na wananchi inayounganisha Nyikonga na Ikunguigazi. Picha na Nicolaus Lyankando

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Jumanne Richard Manyasa licha ya kujivunia mafanikio pia amewaasa wananchi kuendelea kudumisha umoja katika kuleta maendeleo

Sauti ya mwenyekiti

Mgeni rasmi ambaye ni diwani wa kata hiyo Paulo Lutandula amepongeza jitihada za serikali hiyo katika kuleta maendeleo na kusisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano zaidi ili kutatua changamoto zilizobainishwa.

Sauti ya diwani