Storm FM

Tabibu ajiua chumbani kwa rafiki yake

7 April 2024, 5:50 pm

Tukio la kusikitisha katika jamii baada ya tabibu kudaiwa kujiua akiwa chumbani kwa rafiki yake nyakati za usiku.

Na Mrisho Sadick – Geita

Afisa tabibu wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Geita Fimbo Ncheye anadaiwa kujiua akiwa kwenye chumba cha rafiki yake alichokuwa amelala huku akiacha ujumbe wa kuwaomba radhi wazazi wake kwa hatua alizochukua na kutaka mtu yeyote asilaumiwe juu ya kifo hicho.

Ndoto ya tatibu huyo aliyoipambanania kwa muda mrefu imezimika mithiri ya mshumaa, mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mmliki wa nyumba hiyo wamesema limetokea usiku wa kuamkia jana  baada ya kuanza kusikia kelele za mtu kuomba msaada lakini walipofika walikuta kelele zimetulia na walipogonga hakufungua mlango.

Sauti ya Mashuhuda wa tukio
Baadhi ya ndugu wa marehemu wa tabibu aliejiua wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Picha na Mrisho Sadick

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Thomas Mafuru amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema afisa huyo alikuwa akijitolea kwenye kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD) na hakuwa mgonjwa na hakuwahi kueleza iwapo ana tatizo lolote nakwamba hadi sasa hawajafanya uchunguzi kujua chanzo cha kifo chake wanasubiri taratibu za kipolisi pamoja na familia.

Sauti ya mganga mfawidhi Hosptali ya Mji Geita
Hosptali ya mji wa Geita alipokuwa akifanya kazi tabibu huyo. Picha na Mrisho Sadick