Storm FM

Redio jamii sasa kidijitali zaidi

4 July 2023, 3:02 pm

Waandishi wa Habari wakiwa kwenye mafunzo. Picha na Mrisho Sadick.

Kutokana na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano hapa nchini, Mtandao wa Redio za Jamii Tanzania (TADIO) umeendelea kuzijengea uwezo redio hizo ili kujiimarisha kimtandao zaidi.

Na Mrisho Sadick – Geita

Redio za kijamii 11 wanachama wa mtandao wa TADIO kutoka mikoa ya Kanda ya ziwa zimeendelea kujengewa uwezo wa namna ya kuzipa nguvu habari za mtandao kutokana na ukuaji wa teknolojia na idadi kubwa ya watu kuhamia huko.

Mkufunzi wa Redio TADIO Amua Rushita akiwa katika mafunzo hayo jijini Mwanza, amesema idadi kubwa ya watu wanatamani kupata habari kupitia vyanzo vingi ikiwemo kwa sauti , maandishi na picha.

Mkufunzi Amua Rushita akiwajengea uwezo waandishi wa habari wa Redio Jamii. Picha na Mrisho Sadick.
Sauti ya Mkufunzi wa Redio TADIO Amua Rushita
Mkufunzi Hilali Ruhundwa akiwajengea uwezo waandishi wa habari wa Redio Jamii. Picha na Mrisho Sadick

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza Julai 03 hadi 04, 2023 yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Gold Crest Mwanza kwa kuhudhuriwa na Storm FM, Karagwe FM, Kwizera FM, Huheso FM, Sengerema FM, Sibuka FM, Joy FM, Uvinza FM, Uyui FM, Kahama FM na Mazingira FM.