Storm FM

Msako kuanza madereva pikipiki wanaokunja namba za usajili

22 November 2023, 6:25 am

Kaimu Kamanda ACP Adamu Maro akizungumza na wanahabari. Picha na Kale Chongela

Changamoto ya baadhi ya madereva pikipiki kukunja namba za usajili za vyombo vyao imekuwa kubwa kiasi cha Jeshi la Polisi mkoa wa Geita kuingilia kati kwa sababu za kiusalama.

Na Kale Chongela- Geita

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limeanza kufanya msako kwa madereva pikipiki ambao wanakunja namba za usajili kwenye vyombo vyao vya moto.

Wito huo umetolewa na kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Adamu Maro akiwa afisini wakati akizungumza na Storm FM ambapo amesema changamoto hiyo inaleta sintofahamu kwa jamii juu ya dereva kukunja namba hiyo ili isioonekane ilihali namba hiyo ipo jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine inaviashiria vya vitendo vya uharifu .

Aidha Kamanda Maro amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuanza msako kwa madereva wenye tabia hiyo na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.