Storm FM

Geita Queens yazidi kudidimia ligi ya wanawake

25 April 2024, 10:43 am

Goli kipa wa Geita queens (jezi nyeusi) akiwa na mpira baada ya kuokoa shambulizi la Ceasiaa queens. Picha na Juma Zacharia

Ligi kuu ya wanawake Tanzania bara inaendelea ambapo timu mbalimbali za Tanzania zinashiriki katika ligi hiyo

Na Juma Zacharia – Geita

Kikosi cha Geita gold queens cha mkoani Geita kimedondosha alama tatu katika mwendelezo wa ligi kuu ya wanawake Tanzania bara baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya Ceasiaa queens ya mkoani Iringa katika mchezo uliochezwa April 24, 2024 katika uwanja wa Nyankumbu girls mkoani Geita.

Geita gold ilikuwa ya kwanza kuandika goli ndani ya dakika ya pili ya mchezo na baadae Ceasiaa queens kusawazisha na kuongeza goli la ushindi ambapo dakika 45 za kipindi cha kwanza zilikamilika kwa Geita gold queens kuwa nyuma kwa magoli 2-1.

Baada ya kukamilika kwa mchezo huo kocha wa Geita Queens Frank Alloyce amesema matokeo hayo yanaumiza  huku akisisitiza kuwa mpango wao ulikuwa kupata goli la mapema japo wapinzani walisawazisha

Sauti ya kocha wa Geita gold queens

Kwa upande wa Wageni Ceasiaa queens, kocha mkuu wa kikosi hicho Nathan Agwa ameisifia timu yake kwa kuwa ndani ya timu nne za juu katika msimamo akiahidi kuwa haiwezi kushuka daraja.

Sauti ya kochi wa Ceasiaa queens