Storm FM

Mchungaji afariki Dunia akidai atafufuka

12 December 2022, 11:00 am

Na: Mrisho Sadick:

Katika hali ya kushangaza Mtu anaedaiwa kuwa Mchungaji alietambulika kwa jina la Abdiel Raphael mwenye umri wa miaka (42) Mkazi wa Mtaa wa Uwanja kata ya Nyankumbu halmashauri ya mji wa Geita amefariki dunia kwa kile kilichoelezwa kuwa alifunga siku 30 kwa ajili ya maombi katika chumba maalumu kisha akaiambia familia yake kuwa atakufa na baadae atafufuka wasiogope waendelee kufanya maombi.

 Wakazi wa Mtaa wa Uwanja wakiwa Msibani

Mkuu wa kaya alipokuwa akiishi mchungaji huyo Bw Manyasi John amesema aliwaeleza kuwa nyakati za mwisho zimefika nakwamba wafunge maomba ya muda mrefu ndipo yeye akaingia katika chumba kimojawapo katika kaya hiyo nakukaa kwa muda wa siku tatu walipoenda kumuangalia walikuta hali yake siyo nzuri lakini hawakuhofu kitu chochote wakaendelea kufanya maombi kama alivyowaeleza lakini siku tisa baadae wakaanza kuhisi harufu mbaya kutoka katika chumba hicho walipoingia walikuta mwili wake umeanza kuoza.

Mwenyekiti Serikali ya Mtaa Uwanja

Baadhi ya wananchi wa mtaa huo wamesikitishwa na tukio hilo huku Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Uwanja Enosa Chelehani akithibitisha kufariki kwa Mtu huyo nakwamba mwili wake ulikuwa tayari umeshaharibika vibaya ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hosptali ya rufaa ya mkoa wa Geita na shughuli za mazishi zinaendelea ambapo atazikwa katika mtaa wa Mwatulole mjini Geita.