Storm FM

Jamii yakumbushwa kuacha kutumikisha watoto Geita

9 July 2024, 2:41 pm

Wanachama wa CCM tawi la Msalala road mjini Geita katika mkutano wa hadhara. Picha na Edga Rwenduru

Jamii imekumbushwa kuwalinda watoto dhidi a vitendo hatarishi ili kupunguza ukatili ambao unaendelea kwenye jamii.

Imeelezwa kuwa kumekuwepo na ongezeko la watoto wanaoishi mazingira magumu (mitaani) katika mtaa wa Msalala road uliopo kata ya Kalangalala halmashauri ya mji wa Geita huku chanzo kikitajwa kuwa ni wamiliki wa migahawa maarufu kama mama ntilie na wafanyabiashara wa vyuma chakavu kuwatumia katika kazi zao.

Hayo yamebainishwa Julai 8, 2024 na polisi kata ya Kalangalala Emmanuel Mbanga wakati akiwa katika mkutano wa CCM tawi la Msalala road ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mbunge wa jimbo la Geita mji Constantine Kanyasu ambapo Kamanda Mbanga ametoa rai kwa taasisi mbalimbali kusaidia jeshi la polisi kuondoa changamoto hiyo.

Sauti ya Emmanuel Mbanga

Diwani wa viti maalumu halmashauri ya mji Geita Zaitun Swedi Fundikila ametoa rai kwa mama ntilie kuacha kuwatumia watoto hao katika biashara zao.

Sauti ya diwani viti maalumu
Diwani viti maalumu Zaitun Fundikila akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Edga Rwenduru

Mbunge wa jimbo wa jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu amesema amepanga kufanya ziara za kusikiliza kero za wananchi katika kata zote za jimbo la Geita mjini.

Sauti ya mbunge Kanyasu
Mbunge wa jimbo la Geita Constantine Kanyasu akizungumza katika mkutano wa CCM. Picha na Edga Rwenduru