Storm FM

GGML, TAKUKURU zatoa elimu mapambano ya Rushwa

19 April 2024, 10:25 am

Dkt. Omari Mzee kutoka TAKUKURU mkoa wa Geita akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Adelina Ukugani

Tanzania inajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambapo uchaguzi hufanyika kila baada ya miaka mitano.

Na Adelina Ukugani – Geita

Kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa ukaofanyika mwezi oktoba mwaka huu, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) imejipanga kuhakikisha inadhibiti mianya na viashiria vyote vya rushwa ili uchaguzi huo ufanyike kwa misingi ya haki na kuendelea kulinda amani.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU katika warsha iliyoandaliwa na GGML kwa kushirikiana na TAKUKURU mkoani Geita, mkurugenzi msaidizi wa udhibiti kutoka TAKUKURU Dkt. Omari Mzee amesema wamejipanga kuhakikisha mianya na viashiria vyote vya rushwa vinavyoweza kujitokeza vinadhibitiwa.

Sauti ya Dkt. Omari Mzee

Wadau mbalimbali wakiwemo wenyeviti wa mitaa waliojitokeza kupata elimu juu ya rushwa katika warsha iliyoandaliwa na GGML na TAKUKURU mkoa wa Geita. Picha na Adelina Ukugani

Kwa upande wake afisa wa TAKUKURU mkoa wa Geita Maganga Lutunge amesema kuwa moja ya majukumu ya Taasisi hiyo ni kutoa elimu kwa Umma ili kuhakikisha kila mwanajamii anatambua madhara ya rushwa. 

Sauti ya Maganga Lutunge

Baadhi ya wazabuni wanaofanya kazi na kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kusambaza mahitaji mbalimbali ndani ya mgodi huo wamesema GGML inafanya kazi na kila mzabuni ikiwa amefuta sheria kama inavyotakiwa ya upataji wa tenda ndani ya Mgodi.

Sauti ya wazabuni

Warshwa ya utoaji Elimu ya kupambana na rushwa imefanyika kwa muda wa siku nne kuanzia April 15 -18 imeandaliwa na GGML kwa kushirikiana na TAKUKURU mkoa wa Geita ikijipambanua na kaulimbiu isemayo “KUZUIA RUSHWA NI JUKUMU LAKO NA LANGU, TUTIMIZE WAJIBU WETU”