Storm FM

Wasahau mwili wa marehemu ndani nakwenda kuzika jeneza tupu Geita

14 April 2021, 7:41 pm

Na Mrisho Sadick:

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakazi wa mtaa wa Nyantorotoro Kata ya Nyankumbu mjini Geita wamelazimika kuzika mara mbili mwili wa mtoto aliefariki baada ya kutoka kuzika na kuukuta mwili nyumbani.

Tukio hilo limetokea wiki iliyopita, na Mama mzazi wa Mtoto huyo amesema mtoto wake alikuwa na Umri wa miaka (2) aliugua ghafla, kisha akamkimbiza Hospital na baada ya matibabu wakarudi Nyumbani baadae kidogo mtoto huyo akafariki dunia.

Amesema baada ya mtoto huyo kufariki dunia familia ilikaa ikakubaliana  kwenda kumstiri mtoto huyo  wilayani Sengerema Mkoani Mwanza na baada ya mazishi hayo waliukuta mwili huo nyumbani.

Msemaji wa Familia

Kwa upande wake Balozi wa shina namba tatu katika mtaa huo Bw Bundala Edmundi amekiri kuwepo wa tukio hilo nakuongeza kuwa  mazishi ya mtoto huyo yalifanywa kimila nasiyo kidini.