Storm FM

Kero ya barabara yawazidia wana Kilimbu, Msalala

8 October 2023, 3:04 am

Wananchi na Mbunge Iddi katika kijiji cha Kilimbu. Picha na Said Sindo

Licha ya ahadi kadhaa kuendelea kufanyiwa kazi kwa wananchi wa Msalala lakini bado kero ya barabara ni kubwa katika kijiji cha Kilimbu.

Na Zubeda Handrish- Msalala

Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi akiwa katika kijiji cha Kilimbu kata ya Mwalugulu, Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, ameendelea kukutana na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi wake.

Katika mkutano huo wa hadhala wananchi wametoa kero zao ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara.

Sauti ya wanakijiji wa Kilimbu
Wananchi na Diwani katika kijiji cha Kilimbu. Picha na Said Sindo

Nae Diwani wa kata ya Mwalugulu ameelezea jitihada zinazofanyika katika kuendelea kuleta maendeleo na kuwakwamua wananchi kutoka katika changamoto hizo.

Sauti ya Diwani wa kata ya Mwalugulu

Nae Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi amejibia changamoto walizotoa wananchi na suluhisho lake.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi