Storm FM
Storm FM
26 June 2026, 6:17 pm

Leo Juni 26, 2026 TAKUKURU imewafikisha mahakamani watumishi wapatao 18 kutoka katika halmashauri tano za mkoa mkoa wa Geita kutoka na makosa ya ubadhirifu.
Na: Ester Mabula
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita imewafikisha Mahakamani watumishi kumi na nane (18) wa halmashauri za wilaya za Bukombe, Chato, Mbogwe, Nyang’hwale na halmashauri ya manispaa ya Geita kwa makosa ya Ubadhirifu kinyume na K/f cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2023, pamoja na kuisababishia Serikali hasara ya jumla ya shilingi 128,673,342.00 kwa kutokuwasilisha makusanyo tajwa katika akaunti ya makusanyo ya fedha za Serikali kinyume na utaratibu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita James Ruge amewataja watuhumiwa hao kama ifuatavyo:
Watumishi wanne (04) wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ambao ni ; Barthazar Matale Bundala – Afisa Mtendaji Kata ya Uyovu, Marco Nsolo Kabika – Afisa Mtendaji Kijji cha Bulumbaga, Nanzia Chediel Mnzava – Mwandishi mwendesha Ofisi na Peter Paschal John – Mkusanya mapato wa Halmashauri.
Watumishi wawili (02) wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato ambao ni; Nyerembe Bwire Jettah – Mtendaji wa Kata Buseresere na Didacus Malasi Julius – Mtendaji wa Kijiji cha Makurugusi.
Watumishi sita (06) wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ambao ni; Simon Peter
Masanja – Afisa Kilimo, Erasto John Kisusi – Afisa Misitu, Onesmo Stephen Kayombo – Afisa Mtendaji Kata ya Masumbwe, Verius Nestory Bagambisa – Afisa Kilimo wa Kata Lulembela, Aturi Innocent Mutungi – Afisa Kilimo na Mifugo na Christopher A. Mwakeja -Afisa Nyuki Mstaafu.

Watumishi watano (05) wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale ambao ni Mlekwa
Said Mlekwa – Afisa Mtendaji Kata ya Nyugwa, Furaema Malongo Masangwa – Afisa Kilimo Kata ya Busolwa, Joyline Ngaiza Missingo – Afisa Mtendaji Kijiji cha Iseni, Ester Emanuel Manuary – Afisa Mtendaji Kijiji cha Mimbili, Neema Michael Natsey – Mkusanya mapato wa Halmashauri na mwisho ni Mkusanya mapato Yonas Msusa Magesa wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita.
Aidha, Kufuatia matukio hayo, Uchunguzi ulifanyika na baada ya kupata vibali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) watuhumiwa tajwa wamefikishwa Mahakamani leo tarehe 26/06/2026 na kufunguliwa mashauri kumi na nane (18) katika Mahakama za Wilaya za Bukombe, Chato, Mbogwe, Nyang’hwale na Geita ambapo mashauri husika yamesajiliwa.