Storm FM

TAKUKURU Geita yawafikisha kizimbani watumishi 7 kwa ubadhirifu wa fedha

12 June 2026, 4:34 pm

Muonekano wa Jengo la Mahakama ya wilaya ya Geita na Mahakama ya mwanzo Nyankumbu. Picha na Ester Mabula

TAKUKURU mkoa wa Geita imeendelea kuzuia mianya ya Rushwa kwa kuchukua hatua mbalimbali kwwenye makosa mbalimbali kwa kuwafikisha watuhumiwa mahakamani.

Na: Ester Mabula

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita imefanya uchunguzi wa upotevu wa fedha za serikali kupitia mifumo ya ukusanyaji mapato, ambapo kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imewafikisha Mahakamani watumishi wa Umma saba (7) ambao walikusanya mapato kupitia mfumo wa Local Government Revenue Collection Information System- LGRCIS unaotumia mashine za kukusanyia mapato ya Serikali zijulikanazo kama Point of Sale -POS kwa makosa ya ubadhirifu Kif cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007 pamoja na kuisababishia Serikali hasara ya jumla ya Sh. 78,875,110/= kwa kutokuwasilisha makusanyo tajwa katika akaunti ya Serikali kinyume na utaratibu.

Watumishi hao waliohusika na ubadhirifu huu ni: Tatu Jeki Kijungu – Afisa hesabu wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Sylvanus Ngoya Michael- Mhasibu wa Wilaya ya Geita, Ladislaus Katuma Kamhanda- Afisa Mtendaji Kata ya Nyamalimbe Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Melina Damian Buguba-Afisa Uvuvi-Halmashauri ya Wilaya Geita, Mtani Daniel Yangwe- Mkusanya mapato Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Allen Michael Kimaro-Mkusanya mapato Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Mashalla Charles Nkwande-Afisa Mtendaji Kata-Kakubilo-Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Watuhumiwa wa ubadhirifu wa fedha ambao ni watumishi wa UMMA walivyofika mahakamani. Picha na Ester Mabula

Kufuatia matukio hayo na baada ya kupata vibali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) watuhumiwa tajwa wamefikishwa Mahakamani leo tarehe 12/06/2026 na kufunguliwa mashauri saba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita ambayo yamesajiliwa kwa nambari ECO.13145/2026, ECO. 13148/2026, ECO. 13149/2026,na ECO. 13150/2026, ECO. 13151/2026, ECO.13152/2026, ECO. 13153/2026 mtawalia.