Storm FM
Storm FM
15 May 2026, 6:16 pm

“Mtu anafika msibani akiwa amelewa anaanza kuongea mambo ya Simba na Yanga hii haikubaliki si kwa kiongozi hata kwa mtu mwingine yoyote” – Katibu wa maafa
Na: Kale Chongela
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Moringe kata ya Buhalahala halmashauri ya Manispaa ya Geita Bw. Lukas Ngasa ametozwa faini ya kulipa mbuzi mmoja na kamati ya maafa ya mtaa huo baada ya kudaiwa kukiuka taratibu zilizowekwa na kamati hiyo katika utekelezaji wa shughuli katika matukio yanaotokea katika jamii ndani ya mtaa huo.
Akizungumza na Storm FM Katibu wa kamati ya maafa ya mtaa wa Moringe Bw. Aloyce Joseph amesema Bw. Lucas Ngasa alikwenda katika msiba huku akiwa amelewa na kuanza kuzungumza maneno yasiyofaa msibani.
Kwa upande wake, mjumbe huyo Bw. Lukas Ngasa amekanusha tuhuma hizo na kusema kuwa hayupo tayari kutoa faini hiyo ya mbuzi kwani yeye binafsi haoni kosa.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Moringe kata ya Buhalahala manispaa ya Geita Bw. Musa Mabina ameeleza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa inaonesha usawa na uwazi miongoni mwa wana Jamii.