Storm FM

Bilioni 19 kujenga stendi mpya Manispaa ya Geita

6 June 2025, 17:50

Wawakilishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita na kampuni ya SIHOTECH wakionesha mikataba baada ya kusaini. Picha na Kale Chongela

Matamanio ya muda mrefu kwa wakazi wa Manispaa ya Geita yakuahidiwa kituo cha kisasa cha mabasi ya abiria huenda yakafanikiwa baada ya Manispaa hiyo kusaini mkataba wa ujenzi.

Na Kale Chongela:

Halmashauri ya Manispaa ya Geita imesaini mkataba wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha mabasi ya abiria na kampuni ya SIHOTECH Engineering leo Juni 06,2025 EPZA mjini Geita huku ujenzi huo ukitarajiwa kuanza  tarehe 15 ya mwezi huu.
Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Geita Yefred Myenzi akiwa katika hafla hiyo amesema ujenzi huo utagharimu zaidi ya Bilioni 19 ili kuondoa adha waliyokuwa wakiipata wananchi katika kituo cha sasa hususani kipindi cha mvua.

Sauti ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Costantine  Kanyasu  amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia kwa kutoa fedha hizo huku mstahiki meya wa Manispaa hiyo Costantine Morandi amewashukuru wananchi kwa kuendelea kuwa wavulivu kwa kipindi kwa kipindi kirefu.

Sauti ya Mbunge na Meya
Mkuu wa wilaya ya Geita akizungumza katika hafla ya kutia saini mkataba wa ujenzi wa Stendi Kuu ya mabasi Geita mjini. Picha na Kale Chongela

Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Geita amepongeza hatua hiyo huku akimtaka mkandarasi anaetekeleza mradi huo kuhakikisha anazingatia muda wa mkataba kwakuwa kituo kinachotumika kwasasa hakikidhi matarajio.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Geita