Storm FM
Storm FM
7 August 2026, 12:12 pm

Baadhi ya wakina mama waliohudhuria kwenye elimu ya onyonyeshaji kata ya Kasamwa. Picha na Kale Chongela
Wakati wa Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji kuna changamoto ya wanaume kutojitokeza kupata elimu juu ya utoaji wa lishe kwa watoto wao.
Na: Kale Chongela
Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeadhimisha wiki ya Unyonyeshaji ambayo imefanyika katika Kata ya kasamwa ambapo elimu ya lishe Imetolewa kwa wazazi na walezi kwa lengo la kupunguza udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano katika kata hiyo.
Akizungumza na Storm FM Kaimu mganga mkuu manispaa ya Geita akiwa katika kata ya kasamwa Rafael Marko wakati wa Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Bw Rafael Marko amesema Kuna changamoto ya wanaume kutojitokeza kupata elimu juu ya utoaji wa lishe kwa watoto wao.
Sauti ya kaimu mganga mkuu manispaa ya Geita
Afisa Lishe Manispaa ya Geita Bi.Pendo Daniel amesema licha ya maadhimisho hayo kufanyika huduma mbalimbali zimetolewa kwa wananchi ikiwemo upimaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukizwa
Sauti ya afisa lishe manispaa ya Geita

Afisa lishe manispaa ya Geita.Pendo Daniel akiwa anatoa elimu kwa wazazi wanaonyonyesha. Picha na Kale Chongela
Aneth Balinao John akizungumza kwaniaba ya wazazi amesema elimu hii itawasaidia kuwaelimisha wazazi wengine ambao hawajafika katika maadhimisho hayo.
Sauti ya Aneth Balinao John akizungumza kwa niaba ya wazazi wengine
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ambaye ni diwani wa Kata ya Kasamwa Marry Kasanda amewambia lishe aiitaji gharama kubwa kwani ni vyakula ambayo vipo kwenye mazingira yetu ya kila siku.
Sauti ya Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo

Mgeni rasmi Merry Kasanda diwani wa Kata ya Kasamwa akishiriki zoezi la ugawaji wa uji kwa wazazi. Picha na Kale Chongela