Storm FM

Bodi ya GEUWASA yaridhishwa na mradi wa maji wa miji 28 Geita

21 August 2026, 7:59 pm

Wajumbe wa bodi ya GEUWASA wakiwa katika ukaguzi wa mradi wa maji wa miji 28 katika Kata ya Senga wilayani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Mradi unahusisha ujenzi wa mtambo wa kutibu maji wenye uwezo wa lita milioni 44 hadi 45 kwa siku, ujenzi wa mabomba ya kusafirisha maji kwa zaidi ya kilomita 50, pamoja na mtandao wa usambazaji maji wa takribani kilomita 30 ndani ya Mji wa Geita

Na Mrisho Sadick:

Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA) imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Miji 28 unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 124 ambao utawanufaisha Wananchi zaidi ya laki saba wilayani Geita.

Bodi hiyo imetembelea nakukagua maendeleo ya mradi huo wa maji ya Ziwani Victoria Agosti 20,2026 katika Kata ya Senga, Mkurugenzi Mtendaji wa GEUWASA Mhandisi Frank Changawa amesema mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 80 nakwamba utaongeza uzalishaji wa maji hadi kufikia lita milioni 45 kwa siku Kata utahudimia Kata zote 13 za Manispaa ya Geita pamoja na vijiji 19 vya Halmashauri ya Wilaya ya Geita utakamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Wajumbe wa bodi ya GEUWASA wakiwa katika ukaguzi wa mradi wa maji wa miji 28 katika Kata ya Senga wilayani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Mwenyekiti wa Bodi ya GEUWASA  Patricia Samu amesema kukamilika na kuanza kutoa huduma kwa mradi huo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji huku wajumbe wa bodi hiyo Ally Ally na Adelina Kabakama wakitoa wito kwa wananchi kulinda miundombinu ya mradi huo.

Sehemu ya miundombinu ya mradi wa maji wa miji 28 katika Kata ya Senga wilayani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Geita wameiomba serikali kukamilisha mradi huo kwa wakati kwakuwa kwasasa wanakabiliwa na changamoto ya mgao wa maji huku wengine wakitumia vyanzo vya asili ambavyo wakati mwingine maji yake yanakuwa siyo safi na salama.

Taarifa ya Ripoti hii na John Jackson