Storm FM

Sita wafikishwa ofisi ya mtaa kwa uchafu Mwatulole

5 May 2025, 1:55 pm

Wananchi waliofikishwa katika ofisi ya serikali ya mtaa wa Mwatulole kwa uchafu. Picha na Kale Chongela

Kampeni ya HYAGULAGA GEITA ikimaanisha SAFISHA/FAGIA GEITA imeendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ikiwa sambamba na uhamasishaji wa usafi wa maeneo ya Geita.

Na: Kale Chongela – Geita

Watu sita wamefikishwa katika ofisi ya polisi jamii katika mtaa wa Mwatulole kata ya Buhalahala katika halmashauri ya manispaa ya Geita baada ya kubainika maeneo yao ni machafu.

Wakizungumza baadhi ya wananchi hao wamekiri kuwa maeneo yao yamebainika kuwa machafu na kwamba changamoto kubwa ni shimo la choo kujaa hadi kutiririsha maji taka.

Sauti ya wananchi waliokamatwa

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw. Edward Msalaba amekiri watu hao kufikishwa katika ofisi hiyo ambapo amesema baada ya kuwahoji wamekiri maeneo yao kuwa machafu.

Sauti ya mwenyekiti

Ikumbukwe kuwa zoezi hilo ni utekelezaji wa kampeni ya usafi iliyozinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Geita ikiwa na lengo la kuhakikisha usafi unazingatiwa katika maeneo yote.