Storm FM

Maonesho ya nne Geita.

15 September 2021, 5:58 pm

Na Kale Chongela:

Serikali mkoani Geita imewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika sekta ya Madini ambayo yanatarajia kuanza Septemba 16, 2021 katika viwanja vya EPZ mtaa wa Bombambili mjini Geita.

Akizungumza na waandishi wa Ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule amewashauri wakazi wa Geita na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya maonesho hayo Ili kukuza Biashara zao.